• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • v Watu 50 wafariki baada ya treni kuacha njia DRC
  Watu zaidi ya 50 wamefariki dunia baada ya treni ya mizigo kuacha njia mkoani Tanganyika, kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Waziri wa masuala ya kibinadamu Steve Mbikayi amethibitisha habari hiyo na kudokeza kuwa mkutano wa dharura unafanyika ili kupanga mipango ya lazima ya kuwasaidia wahanga.
  Afrika
  • Mwili wa Mugabe wafika Zimbabwe kabla ya mazishi Jumapili 2019-09-12

  Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, aliyekufa nchini Singapore Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 95, umefika Zimbabwe jana Jumatano alasiri kabla ya mazishi yake yaliyopangwa kufanyika Jumapili. Wanasiasa akiwemo rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na mamia ya raia wamepokea mwili wa Mugabe kwenye uwanja wa ndege.

  More>>
  Dunia
  • Iran kukiuka ahadi zaidi za nyuklia 2019-09-12
  Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema nchi yake itachukua hatua zaidi za kusitisha utekelezaji wa ahadi ilizotoa kwenye Makubaliano ya Nyuklia ya Iran (JCPOA) yaliyofikiwa mwaka 2015 kama inahitajika.
  More>>
  China
  • Mwakilishi wa wanawake Hongkong asema wanaojidai kuwa ni "wapiganaji wa uhuru" ni wanafiki wanaotumia vigezo viwili 09-12 09:29
  Akizungumza kwenye kikao cha 42 cha Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea huko Geneva, Bi. Ho amesema yeye na familia yake walishambuliwa, kudhalilishwa na kutishiwa kwenye mtandao wa Internet na wale wanaojidai kuwa ni wapiganaji wa uhuru ambao wanajificha nyuma ya mask na kutothubutu kutaja majina yao ya kweli.
  More>>
  Michezo
  • ULAMA: Mpira wa Mawe kurudi kwa kishindo nchini Mexico
  Kundi la vijana wa Mexico linafufua mchezo wa jadi wa mpira wa mawe kwao maarufu kama 'Ulama', uliowahi kuchezwa na jamii za Aztecs, Maya na Incas.
  More>>
  Makala
  • Biashara kati ya China na nchi za nje yadumisha utulivu

  Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje ilifikia karibu dola trilioni 2.14 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 3.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. Wakati uchumi wa dunia unadidimia na vitendo vya kujilinda kibiashara vinaongezeka, ni vigumu kwa China kupata matokeo hayo mazuri katika biashara ya nje.

  Wiki hii
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 7-Septemba 13)
  1.Nigeria yaanza kuondoshwa raia wake kutoka Afrika Kusini
  2.Mugabe kuzikwa Jumapili
  3.Serikali ya Sudan na makundi ya wapiganaji wakubaliana kufanya mazungumzo ya amani mwezi ujao
  4.Rais wa Kenya asema KDF kuimarisha juhudi za kulinda amani
  5.Rwanda kupokea wakimbizi 500 wa Afrika kutoka Libya hivi karibuni
  6.Misaada zaidi yahitajika kwa ajili ya kukabiliana na wakimbizi wa Somalia
  7.China yatetea utaratibu wa pande nyingi, mazungumzo na ushirikiano kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa
  8.Waziri mkuu wa Uingereza apata uungaji mkono baada ya kura tatu tofauti za maoni kukipa chama chake ushindi
  More>>
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako