• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Santuri za Kichina---Mashairi ya kale ya China 2018-10-01
    Mashairi ya kale ya China ni urithi wenye thamani kubwa sana katika utamaduni wa China, ambayo washairi wa China walieleza matumaini yao kupitia mashairi hayo yenye maneno ya kupendeza yaliyomo, ili kutoa matarajio yao ya kutafuta ukweli, wema na uzuri maishani. Ingawa miaka mingi imeshapita tangu mashairi hayo yalipoanza kuandikwa, lakini bado yanakumbukwa na watu wengi wanaoishi katika zama za hivi leo. Licha ya hayo, kuimba nyimbo zenye mtindo wa kisasa ni njia mpya mwafaka ya kusoma, kufurahia na kueneza mashairi hayo maarufu, ambayo ni njia nzuri ya kuyapatia mashairi hayo ya kale uhai mpya. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo maalumu zilizotungwa kutokana na mashairi ya kale ya China, ili kukufahamisha utamaduni wa mashairi hayo ya China kupitia nyimbo zenye mtindo wa kisasa.
    Santuri za Kichina---Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008 2018-08-08
    Katika tarehe 8 mwezi wa nane mwaka 2008, Michezo ya 29 ya Olimpiki ya majira ya joto ilifunguliwa rasmi mjini Beijing, China, ambayo siku hiyo imekuwa kumbukumbu ya kupendeza isiyosahaulika kwa watu wengi. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zilizoanza kusikika miaka kumi kamili iliyopita kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008.
    Santuri za Kichina---Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina  2018-02-15
    Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina yaani sikukuu ya spring ni sikukuu kubwa kabisa kwa Wachina wote katika mwaka mzima. Kila ifikapo sikukuu hiyo muhimu, watu hurudi nyumbani na kujumuika na familia zao ili kusherehekea mwaka mpya, kwa kuwa nyumbani ni mahali penye furaha na upendo. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo mbalimbali zinazohusu sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina.
    Santuri za Kichina---Mapenzi matamu kati ya wapendanao  2018-02-14
    Tarehe 14 ya mwezi Februari ni siku ya wapendanao. Kila ifikapo siku hiyo maalumu, harufu tamu ya mapenzi inatanda kila pembe ya dunia. Ndiyo ni wakati wa kuburudika na kufurahia hisia ya mapenzi matamu maishani. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu mapenzi matamu kati ya wapendanao.
    Santuri za Kichina---Mwanzo mpya kabisa maishani  2018-01-01
    Mwaka 2018 umefika, mambo mapya yapo kila pembe ya dunia yetu. Tukumbatie kwa pamoja mwaka mpya wa 2018. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu mwanzo mpya kabisa maishani.
    Santuri za Kichina---Miji ya China  2017-12-28
    Miji mingi hapa China inawavutia watalii wengi duniani kuitembelea. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu miji mbalimabli hapa China.
    Santuri za Kichina---Majira ya baridi  2017-12-25
    Majira ya baridi hutujia hapa China kila ifikapo mwishoni mwa mwaka mzima. Theluji huanguka katika majira hayo, ambayo inatupatia dunia yenye mandhari nzuri. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu majira ya baridi.
    Santuri za Kichina---Siku ya Kuzaliwa  2017-12-14
    Siku ya kuzaliwa ni siku maalumu katika mwaka mzima. Furaha na matumaini mengi hutujia katika siku hiyo, ambayo yanabeba penzi kutoka kwa wale wanaotupenda. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu siku ya kuzaliwa.
    Santuri za Kichina---Kukumbuka nyumbani  2017-09-26
    Kuna watu wengi walioko nje ya nyumbani kwa ajili ya kazi au masomo yao, ambao wanakumbuka nyumbani kwao mara kwa mara. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu kukumbuka nyumbani, na kuwatakia watu hao maisha mema na afya njema nje ya nyumbani.
    Santuri za Kichina---Wakati  2017-09-26
    Wakati ni zawadi nzuri kwa kila mtu, ambao unatupatia nafasi nyingi za kutimiza ndoto. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na wakati.
    More>>
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako