• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cristiano Ronaldo atajwa kuwa mchezaji aliyeingiza fedha nyingi zaidi duniani

    (GMT+08:00) 2017-03-30 09:00:01

    Mchezaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa ni mchezaji aliyeingiza fedha nyingi zaidi duniani na jarida la France Football, huku Messi akiwa katika nafasi ya pili kwa msimu wa 2016-17. Ronaldo tayari ameingiza kitita cha pauni milioni 75.62 na amempiga bao mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona ambaye amepata pauni milioni 66.12. Fedha hizo zinatokana na mshahara, posho, malipo ya motisha na mikataba ya matangazo, na Ronaldo anaonekana kupanda haraka baada ya kushinda Ballond'Or.

    Mchezaji mwingine wa Barcelona, Neymar, yeye anaonekana kumpiga bao Gareth Bale wa Madrid. Wachezaji wengine katika orodha hiyo wanao ingiza pesa nyingi zaidi ni pamoja na Gareth Bale wa Real Madrid anayeingiza Pauni milioni 35.4 na Ezequiel Lavezzi anayeichezea Hebei China akiingiza kitita cha Pauni milioni 24.63

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako