• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majeshi ya Afghanistan yaimarisha operesheni na kuwaua wapiganaji zaidi ya 100 wa kundi la Taliban

    (GMT+08:00) 2017-03-30 09:25:29

    Jeshi la Afghanistan limewaua wapiganaji zaidi ya 100 wa kundi la Taliban katika operesheni zilizofanywa kwenye majimbo ya Helmand na Farah.

    Operesheni za jeshi la serikali zimeimarishwa baada ya kundi la Taliban linalodhibiti baadhi ya maeneo ya jimbo la Helmand kutwaa wilaya moja muhimu, na kupanua udhibiti wake.

    Taarifa iliyotolewa na ofisa mwandamizi wa jeshi la serikali inasema moja ya ngome kuu za kundi la Taliban ya Shiwan imebomolewa, na operesheni zitaendelea hadi wapiganaji watakapoondolewa kabisa kwenye eneo hilo.

    Jeshi la serikali pia limesema operesheni kadhaa katika miji Kunar, Kunduz, Baghlan, lakini halikutoa idadi ya wahanga kwa upande wa jeshi la serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako