• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbizi zaidi ya elfu 60 kutoka Sudan Kusini wakimbilia Sudan katika robo ya kwanza mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-03-30 09:58:01

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetangaza kuwa wakimbizi elfu 60 kutoka Sudan Kusini wamefika nchini Sudan katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

    UNHCR imesema idadi ya wakimbizi wapya wanaowasili Sudan imezidi makadirio, hali inayomaanisha kuwa hali nchini Sudan Kusini imezidi kuwa mbaya.

    Mjumbe wa UNHCR nchini Sudan Bi Noriko Yoshida ameitaka jumuiya ya kimataifa iendelee kutoa uungaji mkono kwa Sudan ili kukabiliana na hali ya dharura ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini.

    Mbali na hayo Bi Yoshida ametoa shukrani kwa Sudan kuendelea kufungua mpaka wake na kuwapokea wakimbizi, huku akisema ametiwa moyo kupitia njia ya kuwapatia fursa wakimbizi hao kuishi katika makazi ya huko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako