• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika waazimia kuwa na ngazi sawa ya nishati ya umeme

    (GMT+08:00) 2017-03-30 18:52:13

    Umoja wa Afrika (AU) unafanya juhudi kubwa kuanzisha ngazi sawa kati ya nchi za bara hilo katika nyanja za umeme, elektroniki, na teknolojia zinazohusiana na hizo ili kuhakikisha upatikanaji wa haraka na wa pamoja wa nishati.

    Katibu mtendaji wa Tume ya Kusanifisha Ufundi wa Elektroniki (AFSEC) ya Umoja wa Afrika Bw. Paul Johnson amesema, tume hiyo itawezesha upatikanaji wa pamoja wa nishati barani Afrika na kutimiza ajenda ya Afrika ya mwaka 2063, mfumo unaolenga kutimiza bara lenye mwingiliano, amani, ustawi, na linalofikiria mahitaji ya watu wake.

    Kwa sasa AFSEC ina nchi wanachama 13 na inajaribu kuzikusanya nchi nyingine 55 za Afrika ili kujiunga na mfumo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako