• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania- Rais wa Tanzania asisitiza mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki utakamilika kwa wakati

    (GMT+08:00) 2017-03-30 18:56:21
    Rais wa Tanzania John Magufuli amesisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki unakamilika kwa wakati.

    Aliyasema hayo katika Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokutana na mawaziri wa nishati na madini wa Serikali za Tanzania na Uganda kujadili maendeleo ya mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga, hususan katika masuala ya kikodi yatakayotumika katika mradi huo.

    Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Nishati na Madini, mawaziri hao ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni na ujumbe wake na Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo na wataalamu kutoka serikali zote mbili.

    Aidha, Dk Magufuli aliagiza wawekezaji kutekeleza mradi huo bila kuchelewa kwani serikali imeshaweka mazingira mazuri ya utekelezaji wa mradi, ikiwa ni pamoja na masuala ya usalama, upatikanaji wa ardhi na kodi, hivyo kupunguza gharama za ujenzi Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako