• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Uganda yauza umeme zaidi kwa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-05-11 18:56:28

    Mauzo ya umeme wa Uganda nchini Kenya yameongezeka kwa asilimia 300 ndani ya miezi mine hadi kufikia mwezi Aprili.

    Kenya ilinunua kilowati milioni 92 kutoka Uganda kutokana na kupungua kwa uzalishaji kufuatia kiangazi.

    Taakwimu zinaonyesha kwamba kipindi sawa na hicho mwaka jana Kenya ilinunua kilowati milioni 13 tu.

    Karibu kilowati milioni 910 za umeme wa Uganda unaouzwa Kenya hutoka kwenye vituo vya kuzalisha umeme vya maji.

    Kenya ina laini ya moja kwamoja inaopitia Tororo kwenda Uganda inayowezesha uagiziaji umeme kuwa rahisi.

    Bali na Uganda, Kenya pia huagizia umeme kutoka Ethiopia kutumika kwenye mji jirani wa Moyale.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako