• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sadio Mane awa mchezaji bora wa mwaka wa Klabu ya Liverpool

    (GMT+08:00) 2017-05-12 08:49:16

    Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal na Klabu ya Liverpool, Sadio Mane ameibuka kidedea kwa ushindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Klabu ya Liverpool msimu wa 2016/17 katika hafla zilizofanyika Anfield. Mane ambaye kwa sasa anauguza jeraha la goti, alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo mbili ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu ya Liverpool na Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka chaguo la mashabiki, akimshinda mshindi wa mwaka jana wa tuzo hiyo Mbrazil, Philippe Coutinho.

    Msenegal huyo ameshinda tuzo hizo baada ya kuwa katika kiwango bora tangu alipotua Liverpool mwezi Agosti mwaka jana akitokea Southampton kwa ada ya Pauni Milioni 32. Mpaka sasa Mane ndiye mfungaji bora Liverpool akiwa amefunga mabao 13.

    Wengine waliochomoka na tuzo ni Trent Alexander-Arnold, aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi. Ben Woodburn ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kituo cha kulea na kukuza vipaji kwa vijana cha Liverpool (Academy). Emre Can ametwaa tuzo ya bao bora la mwaka, Lucas Leiva amepewa tuzo ya heshima baada ya kufikisha miaka kumi (10) akiwa klabuni hapo. Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wanawake imeenda kwa Sophie Ingle.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako