• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania na Afrika kusini kushirikiana kupiga jeki maendeleo

    (GMT+08:00) 2017-05-12 16:59:32

    Nchi za Tanzania na Afrika Kusini zimekubaliana kushirikiana katika maeneo 11 ili kupiga jeki ushirikiano wa kimaendeleo kati yao. Ushirikiano huo ni katika biashara, uwekezaji, afya, elimu, sayansi, teknolojia, uchumi wa viwanda, ulinzi na usalama, utalii na madini ambayo yataisaidia Tanzania kukuza uchumi wake.

    Akizungumza baada ya kumpokea mwenzake wa Afrika Kusini, rais John Pombe Magufuli alimuomba raais Zuma ambaye pia ni mwanachama wa jumuiya ya nchi tano zenye nguvu kiuchumi duniani (Brics), kuisaidia Tanzania kupata mikopo nafuu kwa ajili ya kumalizia mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard Gauge. Rais Magufuli amesema ushirikiano huo utasaidia nchi hizo mbili hususani Tanzania katika kukuza uchumi wake. Rais Magufuli amesema nchi hizo mbili zitaendelea kushirikiana katika eneo la biashara na uwekezaji ambapo kwa mwaka jana pekee, biashara kati ya nchi hizo ilifikia thamani ya shilingi 2.4 huku uwekezaji wa Afrika Kusini nchini Tanzania ukifikia dola za kimarekani milioni 800.15 na kutengeneza ajira 20,616.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako