• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Kenya Commercial yatangaza kupungua kwa faida

    (GMT+08:00) 2017-05-12 16:59:47

    Benki ya Kenya Commericial ya Kenya imetangaza kupungua kwa faida ya asilimia 1.9 katika robo ya kwanza ya mwaka huu. Tangazo hilo limakuja wakati ambapo serikali imeweka sheria mpya riba za benki kuwa chini ya asilimia 14. Mkuu wa Benki hiyo Joshua Oigara amesema katika miezi mitatu ya mwanzo wamepata faida ya shilingi bilioni 4.54 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki ambapo walipata faida ya shilingi bilioni 4.63. Baadhi ya mambo yaliyosababisha kupungua kwa faida hiyo ni pamoja na kupungua kwa thamani ya sarafu ya Sudan Kusini na msukosuko wa kisiasa unaoendelea kushuhudiwa nchini Sudan Kusini. Hata hivyo Bwana Oigara amesema benki hiyo imeweka mikakati ikiwemo matumizi ya teknolojia ili kupunguza gharama za oparesheni kwenye benki hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako