• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watanzania wahakikishiwa uwepo wa sukari ya kutosha

    (GMT+08:00) 2017-05-12 17:00:07

    Waziri mkuu wa Tanzania Bwana Kassim Majaliwa amesema Tanzania nchi hiyo ina sukari ya kutosha na kuwataka kuondoa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa bidhaa hiyo. Aidha Majaliwa amewataka wafanyabiashara kutoongeza bei na kuahidi kufuatilia kuhakikisha bei haipandishwi. Kauli hiyo inakuja wiki mbili tu kabla ya waislamu kuanza mfungo wa Ramadhani.Bidhaa hiyo hutumika kwa wingi wakati wa kipindi hicho cha mfungo. Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyiwa za utafiti na Bodi ya Sukari nchini humo, tayari serikali imeagiza tani 80 ambapo tani 35 zimeanzwa kusambaza na nyingine bado zipo bandarini ili kupunguza bei na gharama za sukari.

    Majaliwa ameongeza kuwa serikali imeweka mkakati wa kuongeza uzalishaji katika viwanda vya sukari vya Kagera Sugar, Kilombero, Mtibwa Sugar na TPC Moshi na hata cha Mahonda kisiwani Zanzibar. Majaliwa amesema ili kuondoa tatizo la kuagiza sukari nje ya nchi, amepanga kukutana na wafanyabiashara wa viwanda vya sukari ili viongeze uzalishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako