• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la afya la dunia lathibitisha kuwa ugonjwa wa Ebola umetokea tena nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo

    (GMT+08:00) 2017-05-14 18:27:14

    Shirika la afya la dunia tarehe 13 lilitoa taarifa likisema kuwa serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo iliwasilisha ripoti kwa shirika hilo kuhusu hali ya kutokea ugonjwa wa Ebola nchini humo, hadi kufikia jana iligundua wagonjwa 11 waliohukumiwa kuambukizwa virusi vya Ebola, miongoni mwao watu watatu walikufa, akiwemo mmoja aliyethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

    Hali ya ugonjwa wa Ebola ilitokea mkoani du Bas-Uélé kwenye mpaka kati ya kaskazini ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na jamhuri ya Afrika ya Kati, mgonjwa wa kwanza aliyehukumiwa kuambukizwa virusi hivyo vya Ebola ni mwanamume mwenye umri wa miaka 45, alifariki baada ya kufikishwa hospitalini kwa texi tarehe 22 mwezi Aprili kutokana na hali ya homa ya kihemorajiki. Baadaye, dereva wa texi hiyo na mwuguzi aliyemwangalia mwanamume huyo walifariki.

    Shirika la afya la dunia lilisema kuwa hali mpya ya usambazaji wa ugonjwa wa Ebola hado haijahakikishwa, pande zote zinafanya uchunguzi na tathmini ya hatari, shirika hilo litatangaza matokeo kuhusu hali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako