• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa pendekezo katika mjadala kuhusu utekelezaji wa Makubaliano ya Paris

    (GMT+08:00) 2017-05-14 18:30:47

    Duru ya kwanza ya mjadala wa mwaka 2017 wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa imefanyika huko Bonn, Ujerumani. Mkuu wa ujumbe wa China Bw. Lu Xinming amesema, pendekezo lililotolewa na China limepata ufuatiliaji mkubwa wa nchi zilizoendelea na nchi nyingine zinazoendelea.

    Bw. Lu amesema, katika duru hiyo ya mjadala ujumbe wa China umezingatia kazi za pande nne: ya kwanza ni kuonesha msimamo na pendekezo la China katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kuhimiza mchakato wa pande mbalimbali wa mjadala huo; ya pili ni kuongoza mchakato wa mjadala katika ajenda kuu na kutoa pendekezo la China; ya tatu ni kuimarisha mshikamano na nchi zinazoendelea na kukuzidisha mawasiliano na uratibu ndani ya nchi zinazoendelea ili kulinda maslahi za nchi zinazoendelea; ya nne ni kuimarisha mawasiliano na nchi zilizoendelea na kufanya juhudi kufikia makubaliano katika ajenda kuu.

    Duru ya kwanza ya mjadala wa mwaka 2017 wa Umoja wa Mataifa itakayodumu siku 10 imefunguliwa huko Bonn, wajumbe 4000 hivi kutoka nchi mbalimbali wamehudhuria mjadala huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako