• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi mbalimbali duniani wasifu mkutano wa Ukanda mmoja na Njia moja unaoendelea mjini Beijing China

    (GMT+08:00) 2017-05-14 18:36:03

    Viongozi mbalimbali duniani wamekutana mjini Beijing kwa ufunguzi jukwaa la kimataifa la ukanda mmoja na njia moja na kubadilishana maoni yao juu ya namna bora ya kuendeleza mpango wa ukanda mmoja na njia moja.

    Waziri mkuu waEthiopia Hailemariam Desalegn amesema kuwa huu ni mpango mkubwa usio wa kutatanisha kwa ushirikiano wa kiuchumi katika karne hii ya 21.

    Mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa Mei, Kansela wa Exchequer Phillip Hammond amesema ana imani kwamba Uingereza, kwakua Uingereza ipo magharibi mwishoni mwa ukanda mmoja na njia moja hivyo kwa asili ni mshirika asili wa jitihada hizi.

    Naye mjumbe maalum wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, waziri wa mambo ya uchumi Brigitte Zypries ameeleza kuwa, mkutano huu ni alama ya hatua mpya na maamuzi katika maendeleo ya mpango huo, katika kukabiliana na ukosefu wa miundombinu katika Asia itahitaji juhudi za wale wote wenye mapenzi na walio tayari kuchangia katika ustawi wa kanda nadunia nzima.

    Katika kueleza maoni yake, Rais wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa Peter Thomson amesema mpango wa ukanda mmoja na njia moja utaleta faida kubwa kwa wote wanaohusika juu ya mabadiliko ya kimataifa kama agenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu.

    Naye rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim amesema kuwa utekelezaji wa mpango wa ukanda mmoja na njia moja utasaidia wale walio katika jamii zenye maendeleo, na kueleza kazi kubwa ni kuongeza matarajio ya kukutana na watu wanaoishi katika nchi ambazo bado zinahitaji uwekezaji wa maendeleo zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako