• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Damu inasukumwa na utumbo badala ya moyo mwilini mwa bui bahari

    (GMT+08:00) 2017-07-17 20:03:49

    Kwa wanyama wengi duniani, damu inasukumwa na moyo, lakini bui bahari ni tofauti kabisa, kazi hiyo kimsingi inafanywa na utumbo badala ya moyo.

    Bui bahari ni mdudu anayefanana na bui, ana mwili mdogo na mwembamba, miguu mirefu na myembamba, anaishi pwani, na kuvuta hewa ya Oxygen kutoka maji ya bahari kupitia ngozi yake.

    Wanasayansi wa tawi la Missoula la Chuo Kikuu cha Montana wametoa ripoti kwenye gazeti la Current Biology wakisema tofauti na binadamu, utumbo wa bui bahari uko mwilini kote hata kwenye kila mguu, unafanana zaidi na mfumo wa mzunguko wa damu.

    Viumbe vinavyoishi katika ncha za dunia huwa vikubwa zaidi kuliko vile vinavyoishi katika ukanda wenye halijoto ya wastani au ukanda wa tropiki, hivyo wanasayansi walipofanya uchunguzi katika bara la Antarctic, wamechunguza bui bahari wakubwa wa huko, ili kujua jinsi wanavyovuta hewa ya Oxygen. Uchunguzi na majaribio yanaonesha kuwa moyo ya bui bahari ni dhaifu, hauna uwezo wa kusukuma damu hadi miguuni, lakini utumbo wake una uwezo mkubwa wa kumeng'enya chakula na kupeleka damu na hewa ya Oxygen mwilini kote.

    Watafiti wamesema utumbo wa kipekee wa bui bahari unaonesha kuwa mabadiliko tofauti yametokea kwenye wanyama mbalimbali ili kutatua matatizo yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako