• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yaunga mkono kupunguzwa kwa kikosi cha UN-AU katika Darfur

    (GMT+08:00) 2017-07-20 10:25:55

    Sudan imesema iko tayari kutoa uungaji mkono kusaidia kupunguza idadi ya askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur UNAMID, kwa kushirikiana na kamati za pamoja zilizoundwa kwa ajili hiyo.

    Waziri wa ulinzi wa Sudan Bw. Awad ibn Auf ametoa taarifa baada ya kukutana na naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Bw. Jean-Pierre Lacroix aliyefanya ziara nchini humo, kukagua utekelezaji wa uamuzi huo.

    Bw Ibn Auf amepongeza uamuzi wa Umoja wa Mataifa kupunguza idadi ya askari katika kanda hiyo, na kuitaja hatua hiyo kama ishara ya kuboreka kwa utulivu na hali ya kibanadamu huko Darfur.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako