• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari 16 wameuawa na wapiganaji wa kundi la Taliban kusini mwa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-07-20 18:04:44

    Kundi la wapiganaji wa Taliban limeshambulia vituo vya ukaguzi katika eneo la Kandalan lililoko wilaya ya Sha Walikot mkoani Kandahar, kusini mwa Afghanistan leo alfajiri, na kusababisha vifo vya maafisa 16 wakiwemo askari 10 wa jeshi la nchi hiyo na askari polisi 6.

    Habari zinasema, askari polisi wengine saba wamejeruhiwa, na kwamba wapiganaji kadhaa wa kundi la Taliban pia wameuawa katika mapigano hayo.

    Wakati huohuo, msemaji wa jeshi la polisi mkoa wa Kandahar Zia Durani amethibitisha tukio hilo, lakini hakutoa maelezo zaidi na kusema uchunguzi bado unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako