• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yashuhudia kushuka kwa vifo vinavyotokana na ajali za barabara katika robo ya pili ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-07-20 18:05:01

    Polisi nchini Zambia imesema nchi hiyo imeshuhudia kushuka kwa vifo vinavyotokana na ajali za barabarani katika robo ya pili ya mwaka huu ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka jana.

    Jumla ya watu 432 walifariki katika ajali za barabarani katika robo ya pili ya mwaka huu ikilinganishwa na watu 705 katika kipindi kama hicho mwaka jana, ikiwa ni pungufu kwa 273. Ofisa wa uhusiano wa jamii wa jeshi la polisi Esther Mwaata-Katongo amesema, watu 1,353 walijeruhiwa vibaya katika ajali hizo. Amesema kupungua kwa ajali hizo kunatokana na doria za mara kwa mara, kuzuia usafiri wa umma kufanya kazi muda wa usiku, na kuimarisha matumizi ya sheria za barabarani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako