• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza pendekezo la kuanzisha upya mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2017-07-20 18:11:48

    Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq jana amesema, katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Antonio Guterres amepongeza pendekezo lililotolewa na Korea Kusini la kuanzisha upya mazungumzo kati yake na Korea Kaskazini, pia amewahimiza viongozi wa Korea Kaskazini wajibu pendekezo hilo.

    Bw. Haq amesema, kama alivyosema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres katika mkutano wa mawaziri wa Baraza la Usalama kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea, kukosa njia ya kuwasiliana na Korea Kaskazini ni hatari sana. Amesema kuanza upya na kuimarisha njia ya mawasiliano, hasa kati ya nchi hizo mbili kwenye mambo ya kijeshi, ni muhimu sana kwa kupunguza hatari ya kutoelewana na wasiwasi wa hali ya kikanda.

    Mpaka sasa Korea Kaskazini bado haijajibu pendekezo la Korea Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako