• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Russia, Ukraine, Ufaransa na Ujerumani kufanya mazungumzo kuhusu suala la Ukraine

    (GMT+08:00) 2017-07-20 18:19:16

    Viongozi wa Russia, Ukraine, Ufaransa na Ujerumani watafanya mazungumzo kwa njia ya simu jumatatu wiki ijayo ili kujadiliana kuhusu usalama wa kikanda wa eneo la mashariki mwa Ukraine.

    Hayo yamesemwa na mjumbe maalum wa Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya (OSCE) Martin Sajdik aliposhiriki kwenye mkutano wa kundi la pande tatu za suala la Ukraine. Amesema, ingawa kazi ya kuwatambua wafungwa wa kivita ni ngumu, lakini kazi hiyo imefanywa vizuri.

    Tawi la kundi hilo linaloshughulikia mambo ya usalama limesema, pande husika zimekubaliana kusimamisha vita katika maeneo husika katika majira ya mavuno tangu yaliyoanza tarehe 24 mwezi uliopita hadi tarehe 31 mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako