• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya amani na usalama

    (GMT+08:00) 2017-07-20 19:37:33

    Umoja wa Afrika umesisitiza tena haja ya kuboresha ushirikiano zaidi na Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa katika kuunga mkono uwezo wa Afrika wa kukabiliana na changamoto za amani na usalama.

    Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Kamishna wa Umoja wa Afrika kuhusu Amani na Usalama Bw. Smail Chergui amesema, Umoja wa Afrika ni mshirika wa kutegemeka katika kuimarisha amani na usalama barani Afrika, na unachangia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na changamoto cha usalama duniani.

    Pia kamishna huyo amesisitiza haja ya kuunga mkono uwezeshaji wa maandalizi ya Kikosi cha Dharura cha Umoja huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako