• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Jack Ma's na timu yake ya mabilionea waliingia nchini Kenya kuwinda mikataba 

    (GMT+08:00) 2017-07-20 19:56:56

    Jack Ma, mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa Alibaba, aliinga mjini Nairobi nchini Kenya siku ya Jumatano jioni, kuanzia ziara ya siku mbili.

    Bw; Ma, ambaye ni Mchina, na, ni miongoni mwa wa watu matajiri duniani mwenye thamani ya dola bilioni 30.

    Ameanzia ziara hii leo katika Chuo Kikuu cha Nairobi ili kuongea na vijana wa Kenya kuhusu jinsi ya kujenga na kukuza na kufanikisha biashara zao.

    Wanaume na wanawake 38, kutoka Chama cha Biashara cha Beijing, walioandamana naye katika ziara hii, wanaangalia kuingia katika mikataba ya bilioni ya pesa na serikali ya Kenya na wafanyibiashara wa ndani.

    pia wanatarajiwa kuangalia fursa za biashara katika uchumi mkubwa wa Afrika Mashariki ambako ushawishi wa Kichina umeongezeka kwa kasi, na uwiano wa biashara unapendelea sana kwa China.

    Katibu Mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya Biashara na Maendeleo UNCTAD Mukhisa Kituyi amesema bw Ma atazingatia ufunguzi wa masoko kwa biashara ndogo ndogo na kuhamasisha utamaduni wa biashara Afrika.

    Bingwa wa biashara ya kimataifa, bw: Ma amekuwa akihimiza nchi zinazoendelea kutumia biashara za mtandao e-commerce kuimarisha uchumi wao, badala ya kuweka marshati na kodi ambazo zinaweza kuua sekta inayoibuka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako