Spika wa bunge la umma la China Bw. Zhang Dejiang amekutana na mwenzake wa Gambia Bi. Mariam Denton ambaye yuko ziarani nchini China. Bw. Zhang amesema uhusiano kati ya China na Gambia umefungua ukurasa mpya tangu nchi hizo mbili zirejeshe uhusiano wa kibalozi mwezi Machi mwaka jana, na bunge la umma la China linapenda kushirikiana na bunge la Gambia kutoa mchango wa kuimarisha uhusiano wa pande mbili. Bi. Denton amesema Gambia inathamini uhusiano kati yake na China na itashikilia kithabiti sera ya China Moja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |