• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatunga mpango wa awali wa utafiti wa sayari ndogo

    (GMT+08:00) 2017-09-20 19:35:56

    Kongamano la tatu la kimataifa la Beijing kuhusu utafiti wa mwezi na anga ya juu limefunguliwa leo. Mwanasayansi mkuu wa China wa utafiti wa mwezi Bw. Ouyang Ziyuan, ambaye pia ni mwanachama wa taasisi ya sayansi ya China kwenye kongamano hilo amesema, China inatunga mpango wa awali wa utafiti wa sayari ndogo.

    Kongamano hilo la siku tatu hasa litajadili mipango ya nchi na mashirika muhimu ya kutafiti mwezi, sayari ya Mars na sayari ndogo kabla ya mwaka 2030, hatua zilizopigwa katika utafiti wa sayari na changamoto kuu katika miaka kati ya mitano na kumi ijayo, njia na matokeo ya utafiti wa vitu vilivyochukuliwa kutoka katika mwezi na mahali pengine kwenye anga ya juu, njia mpya za utafiti wa anga ya juu na teknolojia mpya za uchukuzi.

    Kwa mujibu wa waraka wa utafiti wa anga ya juu wa China wa mwaka 2016, katika miaka mitano ijayo, China itatekeleza mpango wa kutafiti sayari ndogo. Mwanasayansi mkuu wa China katika utafiti wa mwezi Bw. Ouyang Ziyuan, ambaye pia ni mwanachama wa taasisi ya sayansi ya China ameeleza kuwa, sayari ndogo ni mabaki ya kuundwa kwa mfumo wa jua, hivyo kwa kutafiti sayari hizo, tutapata ujuzi wa sayansi kuhusu jinsi mfumo wa jua ulivyoundwa, kuna maana sana. Bw. Ouyang amesema China inatunga mpango wa awali wa kutafiti sayari ndogo.

    "Sayari ndogo ziko katika sehemu mbili. Moja ni nje ya sayari ya Mars, na nyingine ni sehemu isiyo mbali na sayari ya dunia. Sayari kwenye sehemu ya pili ni hatari kwetu, kwani ziko karibu na dunia yetu, na zinakimbia bila ya kufuata utaratibu maalumu, ambapo baadhi ya wakati zinagonga dunia. Mpango wa nchi yetu utahusu sayari ndogo za sehemu hizo mbili."

    Kwa kufuata waraka wa utafiti wa anga ya juu wa China wa mwaka 2016, China itafanya safari ya kwanza kwenye sayari ya Mars, na kupiga hatua katika teknolojia ya kuzunguka angani, kushuka na kutembelea sayari hiyo. Mwaka 2020 China itarusha chombo cha kwanza cha kutafiti sayari ya Mars kwa kufika na kuzunguka anga ya sayari hiyo. Mbunifu mkuu wa safari ya kwanza ya sayari ya Mars Bw. Zhang Rongqiao amesema hivi sasa mpango huo unaendelea taratibu..

    "Tumeshaamua malengo ya safari ya mara ya kwanza kwenye Mars, uwezo wa uchukuzi pia umethibitishwa, na kazi ijayo ni kufanya utafiti wa awali kuhusu malengo hayo, ili tuweze kupata matokeo mazuri haraka iwezavyo baada ya kumaliza safari hiyo."

    Tangu mwaka 2004 China ianze utafiti wa mwezi, imerusha vyombo vitatu vya Chang'e No. 1, No. 2 na No.3 vya kutafiti mwezi kwa mfanikio, na kupata vielelezo vingi . Kwa kutumia vielelezo chombo cha Chang'e No. 3 kilizopata, wanasayansi wa China kwa mara ya kwanza walitafiti mchango na ardhi ya mwezi, na kugundua mawe ya aina mpya, mafanikio hayo yamepongezwa na wanasayansi wa nchi nyingine duniani. Bw. Ouyang amesema kutokana na mpango wa utafiti wa mwezi, vyombo vya Chang'e No. 3 na No.4 vitafanya kazi muhimu zaidi.

    "Chombo cha Chang'e No. 5 kitashuka chini kwenye mwezi, baada ya kuchukua mchanga na mawe, kitarudi duniani. Teknolojia kuu ziko tayari, tumefanya jaribio, ambalo limethibitisha kinaweza kushuka katika sehemu tunazotaka kwa usalama. Kwa nini tutarusha Chang'e No. 4? Kwa sababu tunataka kufanya kazi isiyofanywa na binadamu zamani, wajibu wake ni kufika upande mwingine wa mwezi ambao hauonekani kutoka dunia, na binadamu bado hawajafika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako