• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Wajasiriamali wanawake wapewa mafunzo ya kuboresha huduma katika sekta ya utalii

    (GMT+08:00) 2017-09-20 20:54:57

    Zaidi ya wafanyabiashara wanawake 30 katika setka ya utalii wamepewa mafunzo ya kuongeza faida na ushindani.

    Mafunzo hayo yaliyoandaliwa chini ya uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC) yanalenga kuboresha ujuzi wa wanawake katika sekta ya utalii ili kutoa huduma bora.

    Kulingana na Mkuu wa Bodi ya Maendeleo Rwanda Bi Diane Sayinzonga,mradi huo uliopewa jina"Afrika Mashariki:Kuwawezesha wanawake katika biashara" unalenga kuwaunganisha wajasiriamali wanawake katika soko la kimataifaThe training conducted under t.

    Pia mradi huo unalenga kuwawezesha wajasiriamali wanawake kuongeza thamani ya biashara zao za kimataifa,na kuchangia katika lengo la kuongeza mapato na kutoa nafasi za ajira.

    Naibu Mwenyekiti wa chama cha Utalii Rwanda Carol Namatovu,alisema ipo haja ya kuimarisha usawa wa jinsia katika sekta ya utalii ili kuongeza ukuaji.

    Nchini Rwanda utalii unachangia asilimia 4.6 katika pato la taifa na asilimia 30 katika mauzo ya nje ya nchi.

    Mwaka 2016 utalii ulichangia $404 milioni katika ubadilishanaji wa fedha za kigeni.Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB) tayari imetabiri kuwa sekta ya utalii itapata takriban $444 million (about Rwf370 billion) mwaka 2017 kutoka $404 milioni mwaka uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako