• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wafanya kazi kusaidia kuzuia askari watoto nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2017-09-21 08:54:13

    Tume ya umoja wa mataifa nchini Somalia AMISOM imesema imetoa mafunzo wa maofisa 60 wa vikosi vya usalama vya Somalia, ya kuzuia kuandikisha na matumizi ya askari watoto.

    Mwakilishi wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Bw Francisco Madeira, amesema kuna matumizi makubwa ya askari watoto nchini Somalia hasa kwenye kundi la al-Shabaab, na kusema kuna haja ya kutambua idadi halisi ya watoto wanaoshiriki kwenye vita nchini humo.

    Mafunzo hayo yaliyotolewa na tume ya Umoja wa Afrika, yamewahusisha wanajeshi, polisi na idara ya ujasusi, na yamelenga kuwatambua, kuzuia uandikishaji wa watoto na kuwarudisha kwenye jamii waliokuwa askari watoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako