• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa mwingine wa ujasusi wa Somalia auawa katika mlipuko wa mabomu yaliyotegwa kwenye gari

    (GMT+08:00) 2017-09-21 09:01:27

    Ofisa mmoja wa idara ya ujasusi ya Somalia ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika mlipuko wa mabomu yaliyotegwa kwenye gari uliotokea jana katika eneo la Bondere mjini Mogadishu.

    Polisi aliyekuwepo kwenye eneo la tukio hilo amesema ofisa wa shirika la ujasusi na usalama la Somalia NISA Bw Omar Abu Shine ameuawa kwa mabomu yaliyotegwa kwenye gari lake, na uchunguzi kuhusu kifo chake umeanza.

    Wakaazi wamesema ofisa huyo ameuawa akiwa kazini karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu, na kifo chake ni mauaji mapya katika mashambulizi ya kigaidi ya mfululizo yaliyotokea nchini Somalia.

    Kundi la Al-Shabaab limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako