• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema haitakiuka kwanza makubaliano ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2017-09-21 09:14:02

    Rais Hassan Rouhani wa Iran jana kwenye mjadala wa mkutano wa 72 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa alisema Iran haitakiuka kwanza makubaliano ya nyuklia, lakini kama Marekani ikikiuka makubaliano hayo, itajivunjia heshima.

    Rais Rouhani amesema Iran haijawahi kutumia silaha za nyuklia kuzitishia nchi nyingine, na itaendelea kutekeleza makubaliano hayo, pia haitakuwa nchi ya kwanza kukiuka makubaliano hayo. Lakini kama nchi nyingine itavunja makubaliano hayo, Iran itajibu.

    Kwenye mjadala wa tarehe 19, Rais Donald Trump wa Marekani alilaani Iran kutotekeleza makubaliano ya nyuklia, na kusema Marekani haiwezi kutekeleza makubaliano yanayotumiwa kama ngao ya Iran kuendeleza silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako