• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China amesema mageuzi ya operesheni za kulinda amani ni lazima yafuate katiba ya Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2017-09-21 09:14:21

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw Wang Yi jana kwenye mkutano wa ngazi ya juu ya baraza la usalama kuhusu operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, amesema China inaunga mkono kufanya mageuzi ya operesheni za kulinda amani kwenye msingi wa kufuata katiba ya Umoja wa Mataifa, ili operesheni hizo ziwe na ufanisi zaidi.

    Amesema katiba ya Umoja wa Mataifa ni msingi wa operesheni za kulinda amani. Kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa kama vile usawa wa mamlaka ya nchi, kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine na kutatua mgogoro kwa njia ya amani, pamoja na mwongozo wa operesheni za kulinda amani, ni lazima zitekelezwe kihalisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako