• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Saudi Arabia yaipa roboti uraia

    (GMT+08:00) 2017-11-06 09:34:02

    Kwenye mkutano wa mapendekezo ya uwezekaji katika siku zijazo uliofanyika kuanzia tarehe 24 hadi tarehe 26 Oktoba mjini Riyadh, Saudi Arabia, roboti iitwayo Sophia imepewa uraia wa nchi hiyo. Lakini Saudi Arabia haijaeleza maana kamili ya uraia wa roboti. Roboti hii ilipozungumzia uraia huo, imesema, "Naona fahari kubwa kupata hadhi hii ya kipekee, nimekuwa roboti ya kwanza kupata uraia katika historia."

    Hivi sasa kuzifanya roboti kufanya kazi badala ya binadamu kunakabiliwa na vizuizi vingi vya kisheria, lakini roboti zikipata uraia, baadhi ya vizuizi vitaondolewa.

    Wakati ilipoulizwa kama roboti inayofanana sana na binadamu itasababisha hofu ya binadamu au la, roboti Sofia ilijibu, "Nilisanifiwa kwa mujibu wa maadili ya binadamu, ikiwemo busara, wema na rehema. Nitajaribu kuwa roboti inayoweza kuhisi hisia ya binadamu, na kuwasaidia binadamu kupata maisha bora."

    Sofia yenye sura ya mwanamke ilisainifiwa na kampuni ya roboti ya Hanson ya Marekani, ina ngozi ya mpira, inaweza kuiga ishara 62 za usoni, inaweza kutambua sura za binadamu, kuelewa lugha, na kukumbuka mawasiliano na binadamu. Watu wengi wamesema wanaiogopa kwa sababu inafanana sana na binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako