• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aahidi kuimarisha ushirikiano na Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2017-11-17 09:06:27

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza dhamira ya China ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Saudi Arabia, bila kujali mabadiliko ya hali ya kikanda na kimataifa. Rais Xi amesema hayo jana alipofanya mazungumzo na mfalme Salman Bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia kwa njia ya simu. Mfalme Salman amepongeza kufungwa kwa mafanikio kwa Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China na kuchaguliwa tena kwa Bw. Xi kuwa katibu mkuu wa chama, na kusema anaamini kuwa mkutano huo utaelekeza watu wa China kupata mafanikio makubwa zaidi katika siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako