• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa nne wa kimataifa wa mtandao wa Internet kufanyika Disemba, China

    (GMT+08:00) 2017-11-17 17:36:40

    Mkutano wa nne wa kimataifa wa mtandao wa Internet utafanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 mwezi ujao, huko Wuzheng, mkoani Zhejiang. Madhumuni ya mkutano huo wenye kauli mbiu "kuendeleza uchumi wa kidijitali, na kuhimiza ufunguaji mlango na kunufaika kwa pamoja----kushirikiana kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya mtandao wa Internet", ni kujumuisha mafanikio ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia mpya, kuchangia busara kwa ajili ya maendeleo na usimamizi wa mtandao wa Internet, na kufikia makubaliano. Hivi sasa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika.

    Tangu mwaka 1994 ijiunge na mtandao wa Internet, China imekuwa nchi yenye ushawishi mkubwa katika shughuli za mtandao huo baada ya maendeleo ya zaidi ya miaka 20. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana, naibu mkurugenzi wa ofisi kuu ya habari za mtandao wa Internet ya China Bw. Ren Xianliang amesema, uchumi wa kidijitali ni mafanikio makubwa zaidi yaliyopatikana kutokana na maendeleo ya mtandao wa Internet nchini China.

    "Katika miaka kadhaa iliyopita, maendeleo ya uchumi wa kidijitali yamejitokeza, na kusukuma mbele shughuli za uvumbuzi wa uchumi mzima. Mwaka jana thamani ya uchumi wa kidijitali nchini China ilifikia renminbi yuan trilioni 22.4 sawa na dola za kimarekani karibu trilioni 3.8, na kuchukua asilimia 30.1 ya thamani ya jumla ya uzalishaji mali nchini China, huku biashara kwa njia ya mtandao wa Internet ikifikia yuan trilioni 26 sawa na dola za kimarekani zaidi ya trilioni 3.9. Wakati huo huo, idadi ya watumiaji wa mtandao wa Internet nchini China imefikia milioni 750, na wastani wa ongezeko kwa mwaka la mauzo ya rejareja kwenye mtandao huo ni asilimia 30."

    Kutokana na hali hizo, kwenye mkutano huo, licha ya kongamano kuu la ufunguzi, maonesho, mkutano wa matangazo ya matoleo mapya, pia kutakuwa na makongamano 20 madogo kuhusu uchumi wa kidijitali, teknolojia ya kisasa, uhusiano kati ya mtandao wa Internet na jamii, usimamizi wa mtandao wa Internet na mawasiliano na ushirikiano wa shughuli zinazohusika. Alipozungumzia mvuto wa mkutano huo, Bw. Ren Xianliang anasema,

    "Kwanza ni kutilia mkazo uvumbuzi. Mkutano huo umeongeza "majadiliano kuhusu teknolojia za hali ya juu zaidi za mtandao wa Internet", ili kufuatilia mwelekeo mpya wa mtandao wa Internet duniai katika siku za baadaye, pia umeweka mada za roboti na uchumi wa kuchangia matumizi. Pili ni kuonesha manufaa kwa watu wote. Mkutano huo pia umeongeza mazungumzo kuhusu "uhusiano kati ya mtandao wa Internet na jamii", ili kufuatilia matumizi ya mtandao huo katika juhudi za kupunguza umaskini na maafa, na kulinda utamaduni kwa kulingana na malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa."

    Mkutano huo umeandaliwa kwa kushirikisha shirikisho la kimataifa la upashanaji habari wa simu za mkononi na shirikisho la kimataifa la haki miliki, ili kuongeza uwakilishi wa kimataifa.

    Naibu mkurugenzi wa tume ya maandalizi ya mkutano huo Bi Ge Huijun amesema, mvuto mwingine wa mkutano huo ni maonesho ya teknolojia za hali ya juu zaidi za mtandao wa Internet. Anasema,

    "Kampuni maarufu zikiwemo Alibaba, Baidu, Huawei, SAP ya Ujerumani na Kaspersky zitaonesha matoleo yao mpya na ya hali ya juu zaidi. Kwenye mkutano huo pia tutaonesha vitu vingine vipya vikiwemo supamaketi isiyo na wahudumu, vifaa vya tafsiri, roboti inayoongozwa kutoka mbali, upashanaji habari wa Quantum."

    Mkutano huo pia utatoa ripoti mbili kuhusu maendeleo ya mtandao wa Internet nchini China na dunia nzima katika mwaka 2017, ambazo zitaonesha hali ya sasa na mwelekeo wa maendeleo ya mtandao huo nchini China na duniani.

    Hivi sasa China imemaliza kimsingi kazi za maandalizi ya mkutano huo utakaohudhuriwa na wajumbe 1,500 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

    Bw. Ren Xianliang amesema China itafungua mlango zaidi, na kuzikaribisha kampuni za mtandao wa Internet za nchi mbalimbali duniani kuanzisha shughuli nchini China ili kunufaika na maendeleo nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako