• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Biashara zapungua Uganda kutokana na siasa za Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-17 18:52:12

    Sekta ya kibinafsi nchini Uganda imesema biashara zao zimepungua kidogo kutokana na hali ya kisiasa ya nchi jirani ya Kenya.

    Ripoti ya benki ya Stanbic inaonyesha kuwa sekta zilizoathiria ni zile za kilimo, huduma, ujenzi, na maduka ya mauzo ya jumla.

    Mchumi wa kikanda kwenye benki hiyo Jibran Qureishi, amesema tangu mwezi Agosti kumekuwa na udhaifu katika ukuaji wa sekta hizo.

    Uganda ambayo ni mshirika mkuu wa kibiashara wa Kenya inatakeleza miradi mikubwa ya miundo mbinu na inahitaji kupitisha malighafi kupitia bandari ya Mombasa.

    Lakini kutokana na msimu wa siasa nchini Kenya michatako ya kusafirisha bidhaa kutoka Mombasa hadi Uganda imekuwa ikiathirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako