Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, China inazitaka pande mbalimbali za Zimbabwe zizingatie maslahi ya kimsingi na ya muda mrefu, na kutatua masuala husika kwa amani na mwafaka.
Bw. Geng Shuang amesema, hivi sasa nchi wanachama wa SADC zimechukua hatua za usuluhishi. China inazitaka pande mbalimbali za Zimbabwe kushikilia kufanya mazungumzo, kuondoa migongano, kuhimiza masuala husika kutatuliwa kwa amani na mwafaka chini ya msingi wa kisheria, na kulinda utulivu wa taifa na utaratibu wa jamii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |