• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riadha, Caster Semenya wa Afrika Kusini atajwa kuwania tuzo ya mwanamichezo bora duniani

    (GMT+08:00) 2018-01-18 08:15:35
    Bingwa wa riadha kwa upande wa wanawake nchini Afrika Kusini Caster Semenya ametajwa kuwania tuzo ya mwanamichezo bora kwa upande wa wanawake duniani kwa mwaka 2017, tuzo zinazojulikana kama Laureus World Sports Woman of the Year Award itakayotolewa mjini Monaco nchini Ufaransa Februari 27 mwaka huu.

    Katika tuzo hiyo kwa mwaka huu Caster anashindana na nyota wengine duniani wakiwemo, wachezaji wa tennis Serena Williams wa Marekani, Garbine Muguruza wa Hispania, bingwa wa michezo ya kuteleza kwenye barafu Mikaela Shriffin wa Marekani na Chipukizi nyota katika mchezo wa kuogelea kutoka Marekani.

    Akitoa pongezi za serikali, Rais wa chama cha riadha cha Afrika Kusini, Alech Skhosana, pamoja na mambo mengine, amesema taifa zima lina imani na Caster, vile vile linaamini atatwaa tuzo hiyo, huku akimshukuru kocha wa mwanamichezo huyo ambaye ni bingwa mara tatu wa mbio za mita 800 wanawake duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako