Korea Kusini na Korea Kaskazini zimekubaliana kuunda ujumbe wa pamoja chini ya bendera ya pamoja ya peninsula ya Korea kwenye gwaride la ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi , itakayofanyika mwezi ujao mjini PyeongChang nchini Korea Kusini. Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mazungumzo ya manaibu mawaziri kwenye eneo la usalama lililoko kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |