• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa ujenzi wa China ya kidigitali kufanyika mwezi ujao

    (GMT+08:00) 2018-03-22 17:30:44

    Mkutano wa kwanza wa kilele wa ujenzi wa China ya kidigitali utafanyika mwezi Aprili, mjini Fuzhou China. Mkutano huo utaonesha matokeo mapya ya ujenzi wa China ya kidigitali yaliyopatikana katika miaka ya hivi karibuni kupitia sanifu za mitindo mipya ya shughuli za kisiasa za kielektroniki, na mchanganyiko wa kina wa uchumi wa kidigitali na maisha ya jamii.

    Kauli mbiu ya mkutano wa kwanza wa kilele wa ujenzi wa China ya kidigitali ni "kuhimiza mambo ya kisasa kwa mambo ya habari, na kuharakisha kujenga China ya kidigitali. Madhumuni ya kufanya mkutano huo ni kutoa jukwaa la kutangaza sera za maendeleo ya mambo ya habari, na jukwaa la kuonesha matokeo ya maendeleo ya shughuli za kisiasa za kidigitali na uchumi wa kidigitali.

    Naibu mkuu wa mkoa wa Fujian Bw. Zhang Zhinan leo kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, mkutano huo utaonesha kiwango cha maendeleo ya teknolojia za kidigitali nchini China. Anasema,

    "Teknolojia za mifumo ya utambuzi wa sura na sauti, kulipa bila ya pesa halisi, ukaguzi bila ya kugusa, magari yanayojiendesha na nyinginezo zitatumika katika mkutano huo. Tunatumai watu watapata hisia mpya."

    Mkoa wa Fujian ni mmoja kati ya mikoa iliyoanzisha mapema shughuli za kidigitali na ujenzi wa uchumi wa kidigitali. Baada ya juhudi za miaka mingi, "ujenzi wa Fujian ya kidigitali" umepata mafanikio dhahiri. Miji yote ya mkoa huo ina mtandao wa 4G wa simu za mkononi, na huduma za mtandao mpana wa Internet, hata wakazi wa vijijini wanaweza kupata huduma ya mtandao wa internet. Bw. Zhang anasema,

    "Tunapenda kugawanya matokeo yetu. Tumeweka mifumo karibu elfu moja ya idara zetu za serikali ya kushughulikia mambo kwenye tovuti za mtandao, hali ambayo inaweza kuwasaidia wengine kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa."

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari, naibu mkurugenzi wa ofisi ya shughuli za mtandao wa Internet ya China Bw. Zhuang Rongwen amesema, mkutano huo pia utatangaza majaribio mazuri zaidi ya ujenzi wa China ya kidigitali ya mwaka huu, na kufuatilia shughuli za kisiasa ya kidigitali. Amesema kwa hatua ijayo China itahimiza habari za shughuli za kisiasa ziwe wazi zaidi, na kugawanya habari za kidigitali.

    "Tutajitahidi kuanzisha jukwaa la kitaifa kwenye mtandao wa Internet mwishoni mwa mwaka huu, na kufungua baadhi ya habari za kiserikali. Hadi kufikia mwaka 2020, habari zote muhimu za serikali zitafunguliwa kwa umma."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako