• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Biashara ya makaa kupigwa marufuku

    (GMT+08:00) 2018-03-22 19:36:04
    Kenya imejiunga na ulimwengu leo kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuhifadhi misitu huku taifa hili lilikabiliwa na uharibifu mkubwa wa misitu unaosababishwa na ukataji miti kiholela.

    Madhimisho ya siku hiyo mwaka huu yamefanyika kwenye msitu wa Karura ambapo waziri wa mazingira Keriako Tobiko anawaongoza Wakenya kupanda miche elfu-10 kama sehemu ya juhudi za kuongeza misitu humu nchini.

    Kauli mbiyu ya siku hiyo mwaka huu ni "misitu kwa miji endelevu" na inaangazia jinsi miti katika maeneo ya miji inavyoweza kudhibiti viwango vya joto, kuimarisha utoaji maji, kutoa lishe bora na makazi, kusafisha hewa na kuimarisha utangamano wa kijamii miongoni mwa masuala mengine.

    Umoja wa Mataifa uliratibisha tarehe 21 mwezi Machi kuwa siku ya kuhifadhi misitu mnamo mwaka 2012.

    Siku hii huadhamishwa kwa kuangazia na kutoa hamasisho kuhusu umuhimu wa misitu kwa binadamu

    Wakati wa maadhimisho hayo, serikali huhimizwa kuchukua juhudi za kitaifa na kimataifa za kuandaa shughuli mbalimbali za upanzi miti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako