• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Cameroon zakubaliana kuimarisha uhusiano

    (GMT+08:00) 2018-03-22 20:48:54

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amefanya mazungumzo na mwenzake wa Cameroon Paul Biya, ambapo marais hao wawili wamekubaliana kutumia nguvu bora za urafiki wenye msingi imara na ushirikiano mkubwa ili kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwenye kiwango kipya.

    Rais Xi Jinping amesema, China inakaribisha Cameroon kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kushirikiana na China kuhimiza uhusiano wa kimataifa wa aina mpya wa kuheshimiana, haki, usawa na ushirikiano wa kunufaishana, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.

    Kwa upande wake, Rais Biya amempongeza rais Xi Jinping kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa China. Amesema, Cameroon inasifu pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na inaunga mkono ushirikiano ndani ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako