• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe awasamehe wafungwa 3,000

    (GMT+08:00) 2018-03-23 09:51:52

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amewasamehe wafungwa 3,000 ikuwa ni hatua ya serikali kupunguza msongamano magerezani, na na kuboresha hali ya maisha ya wafungwa.

    Habari kutoka idara ya usimamizi wa magereza ya Zimbabwe zinasema waliopewa msamaha huo ni wanawake wote, isipokuwa wale waliohukumiwa adhabu ya kifo na wenye vifungo vya maisha, wafungwa wadogo na wale waliofungwa kwa muda wa chini ya miaka 3, wafungwa walemavu, wagonjwa mahututi na wazee wenye umri zaidi ya 60.

    Msamaha huo ni msamaha wa kwanza wa Rais Mnangagwa tangu aingie madarakani mwezi Novemba, na unatokana na upungufu wa fedha kwa magereza ya Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako