• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yaahidi kuwawezesha watu wote wanufaike na utoaji wa huduma za afya

    (GMT+08:00) 2018-05-22 16:57:20

    Mkutano wa 71 wa afya duniani ulifunguliwa jana mjini Geneva, Uswisi. Katibu mkuu wa shirika hilo Bw. Tedros Ghebreyesus ametoa Mipango mikuu ya 13 ya WHO katika miaka mitano ijayo. Mkurugenzi wa Kamati ya afya ya China Bw. Ma Xiaowei ameshiriki kwenye mkutano akiongoza ujumbe wa China.

    Mkutano wa afya duniani ni mkutano muhimu zaidi wa WHO, wawakilishi wa nchi zote 194 wanachama wa shirika hilo watajadili masuala muhimu kuhusu afya ya umma duniani ikiwemo Mipango mikuu ya 13 ya WHO. Waziri wa afya wa Zimbabwe Bw. David Parirenyatwa akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano huo, amesema lengo la maendeleo endelevu kwa WHO ni kutoa huduma za afya kwa watu wote kabla ya mwaka 2030, na kutoa ahadi kuchukua hatua za lazima ili kutimiza lengo hilo. Bw. Parirenyatwa anasema:

    "Ajenda ya mkutano huo ni kutoa huduma kwa watu wote. Kazi kuu ya mkutano huo ni kujadili na kuthibitisha Mipango mikuu ya 13 ya kazi, ambayo itaelekeza kazi ya WHO katika miaka mitano ijayo."

    Mpango huo uliotajwa na Bw. Tedros unalenga kuwezesha ongezeko la idadi ya watu wanaonufaika na huduma za afya, kupewa ulinzi zaidi wanapokabiliwa na matukio ya dharura ya afya, na kuboreshwa utoaji wa huduma za afya. Bw. Tedros anasema:

    "Kuwa na shirika lenye nguvu kubwa zaidi la afya, utoaji wa ahadi za kisiasa na uhusiano wa kiwenzi, ni vipaumbele vitatu vya kazi kwa WHO, na utoaji wa huduma kwa watu wote ni msingi wa kazi zote."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako