• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Ongezeko la bei ya petroli kwazua hofu ya ongezeko la bei za bidhaa

    (GMT+08:00) 2018-05-22 21:10:32

    Benki kuu za Afrika Mashariki zinakisia kwamba huenda bei za bidhaa zikaongezeka kipindi hiki kilichosalia kwa mwaka huu, kutokana na kuongezeka kwa bei ya petrol kimataifa. Hii ni kando na kuongezeka kwa ushuru unaotozwa kwa bidhaa hii muhimu na baadhi ya mataifa. Gavana wa Benki kuu ya Uganda Emmanuel Tumusiime Mutebile amesema kwamba bei ya bidhaa itaongezeka pole pole kutokana na mipango ya kuongeza ushuru unaotozwa uagizaji wa mafuta ya petroli kutoka nje. Bei ya bidhaa nchini Uganda ilipungua kwa asilimia 1.8 mwezi April, kutoka asilimia 2 mnamo mwezi Machi. Hii ilitokana na kupungua kwa bei ya vyakula. Hata hivyo kuna wasiwasi kuwa bei itapanda tena kutokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta ya petrol.

    Nchini Tanzania, bei ya bidhaa ilipungua kwa asilimia 3.8 mnamo mweiz Aprili, kutoka asilimia 3.9 mnamo mwezi Machi. Vile vile, huenda mambo yakwa mabaya kutokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta.

    Mambo ni sawa na hayo nchini Kenya, ambapo bei ya bidhaa ilishuka kutoka asilimia 11.48 mnamo mwezi Aprili mwaka uliopita hadi asilimia 3.73 mwezi wa Aprili mwaka huu. Hata hivyo Benki kuu ya Kenya inasema kuwa, malengo ya seruikali kuu ni kuhakikisha kuwa bei ya bidhaa itasalia kati ya asilimia 2.5 na asilimia 7.5, endapo bei ya mafuta itapanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako