• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Vijana na akina mama wapigwa jeki na serikali

    (GMT+08:00) 2018-05-22 21:11:20

    Shilingi milioni 25.3 pesa za Tanzania, zimetolewa kwa njia ya mkopo ili kuwafaa vijana na makundi ya wanawake. Kauli hii imetolewa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege wakati akijibu swali la mbunge wa Buhigwe Albert Obama, aliyetaka kujua ni lini serikali itasaidia mitaji makundi hayo, ili waweze kujikwamua kiuchumi.

    Waziri Kandege amesema kwamba Halmashauri ya Buhigwe ilianza kuwajibika mnamo mwaka wa 2013, na kuanzia wakati huo, pesa zimekuwa zikitolewa.

    Amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 20.2 zimetengwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa makundi ya vijana na wanawake. Ameongeza kuwa ni lazima pesa hizo ziwafikie wahusika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako