• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNECA kufanya mkutano kuhusu biashara ya kidigitali barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-05-23 10:06:32

    Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA imesisitiza kutafuta fursa za biashara za kidijitali chini ya utaratibu wa Eneo la Biashara Huria barani Afrika AfCFTA.

    UNECA imesema imeandaa mkutano wa ngazi ya juu uitwao "Biashara ya Kidijitali Barani Afrika: Athari kwa Ujumuishi na Haki za Binadamu". Mkutano huo unaopangwa kufanyika kuanzia Mei, 31 hadi Juni,1 katika makao makuu ya UNECA mjini Addis Ababa unatarajiwa kuwakutanisha wataalamu wa ngazi juu kuhusu biashara ya kidijitali barani Afrika.

    Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, fursa za biashara ya kwenye mtandao wa internet zimewezesha sekta mbalimbali kupata masoko, wateja na bidhaa barani Afrika, na thamani ya biashara ya aina hiyo barani humo inatarajiwa kufikia dola za kimarekani bilioni 50 hadi bilioni 75 kwa mwaka katika miaka mitano hadi kumi ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako