• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 25 wafariki baada ya kimbunga cha Sagar kulikumba jimbo la Somaliland

    (GMT+08:00) 2018-05-23 10:06:54
    Watu wasiopungua 25 wamefariki na wengine 27 hawajulikani walipo baada ya kimbunga cha Sagar kulikumba eneo la Somaliland, kaskazini mwa Somalia na kusababisha mvua kubwa na mafuriko.

    Takwimu zilizotolewa na mamlaka za Somaliland zinaonyesha kuwa, watu 12 wakiwemo watoto wamejeruhiwa katika maafa hayo. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais pia inasema familia laki 1.6 zilizopo kwenye eneo la pwani zimeathiriwa na kimbunga hicho.

    Shirika la hisani la kimataifa Save the Chidren limeonya kuwa hali ya maisha ya watoto itakuwa mbaya zaidi kutokana na ukosefu mkubwa wa chakula, kupoteza makazi na magonjwa yanayoweza kuenea kwa maji baada ya maafa hayo kutokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako