• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WFP yaisifu China kwa kutoa msaada wa chakula kwa Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-05-23 10:40:52

    Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP limeipongeza China kwa kutoa msaada wa chakula kwa watu wenye mahitaji nchini Sudan Kusini.

    Msaidizi wa mkurugenzi mtendaji wa WFP anayeshughulikia operesheni Bibi Valerie Guarnieri, amesema hivi sasa watu zaidi ya milioni 7 hawana chakula cha kutosha nchini Sudan Kusini, na msaada wa chakula uliotolewa hivi karibuni na China unaweza kuwaokoa maelfu ya watu wenye njaa.

    Bibi Guarnieri ameyasema hayo kwenye hafla ya kukabidhi tani zaidi ya elfu mbili za mchele zilizotolewa na China kwa WFP. Mchango huo ni sehemu ya tani 8,800 za mchele zilizoahidiwa na China kwa Sudan Kusini mwaka jana, ili kupambana na ukosefu wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako