v Balozi wa China nchini Rwanda asema ziara ya rais Xi nchini Rwanda itahimiza uhusiano kati nchi hizo mbili
Kutokana na mwaliko wa rais Paul Kagame wa Rwanda, rais Xi Jinping wa China ataanza ziara yake rasmi nchini Rwanda tarehe 22 hadi tarehe 23 Julai. Kabla ya ziara hiyo, balozi wa China nchini Rwanda Bw. Rao Hongwei aliwaambia wanahabari wa nchi hizo mbili kuwa, ziara hiyo ya rais Xi Jinping itahimiza uhusiano kati ya China na Rwanda uingie kwenye zama mpya, na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.
|