• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping awasili Abu Dhabi kwa ziara rasmi nchini UAE

    (GMT+08:00) 2018-07-20 10:12:06

    Rais Xi Jinping wa China amewasili Abu Dhabi na kuanza ziara yake ya kiserikali nchini Umoja wa Falme za Kiarabu UAE.

    Kwenye uwanja wa ndege, Rais Xi Jinping na mkewe Bibi Peng Liyuan wamekaribishwa na waziri mkuu wa UAE Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum pamoja na Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan.

    Rais Xi amesema katika miaka hiyo 34 tangu nchi hizo mbili zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, pande zote mbili zimeheshimiana na kutendeana kwa usawa, uhusiano wa pande mbili umeendelea vizuri, na ushirikiano wa kiutendaji kwenye sekta mbalimbali umepata mafanikio. Amesema UAE ikiwa ni kituo cha kwanza katika ziara yake, inamaanisha kuwa China inatilia maaani uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Viongozi hao wa Umoja wa Falme za Kiarabu wamesema rais Xi ni rafiki mkubwa wa wananchi wa UAE, na wanatarajia ziara hiyo ya kihistoria, itahimiza maendeleo ya uhusiano wa kimkakati kati ya pande mbili.

    Baada ya kumaliza ziara nchini UAE, rais Xi atafanya ziara nchini Senegal, Rwanda na Afrika Kusini ambako pia atahudhuria Mkutano wa kilele wa BRICS mjini Johannesburg. Rais Xi pia anatarajiwa kutemebelea Mauritius akiwa njiani kurudi nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako