• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siri ya makampuni ya Marekani kupata faida kwenye biashara zao nchini China

    (GMT+08:00) 2018-07-20 10:50:15

    Kamati ya kipengele cha 301 cha Sheria ya biashara ya Marekani itakutana kuanzia Agosti 20 hadi 23 kujadili orodha iliyotolewa Julai 10 na serikali ya Marekani ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 ambazo zitatozwa ushuru wa asilimia 10. Serikali ya Trump imesema, hatua hiyo inatokana na mienendo isiyo ya haki ya China kwenye biashara, ambayo imeisababishia Marekani hasara kubwa.

    Lakini madai hayo si ya kweli.

    Kwanza, kutokana na ukuaji wa kasi wa uchumi wa China na soko lake kubwa, mashirika mengi ya Marekani yamepata mafanikio makubwa kwenye biashara zao nchini China, kwa mfano kampuni ya simu za mkononi ya Apple, kampuni ya magari ya General motors n.k.

    Pili, ili kuhamasisha makampuni ya nje kuwekeza kwenye maeneo yaliyo nyuma kimaendeleo nchini China, au kuwekeza kwenye sekta zinazopewa vipaumbele, serikali ya mitaa ya China imeweka sera nyingi nafuu kwa makampuni ya nje kwenye mambo ya fedha na kodi, mitaji na ardhi. Kwa makampuni ya Marekani yaliyowekeza nchini China, sera hizo si kama tu ni msukumo muhimu wa maendeleo yao, na bali pia ni chanzo kikubwa cha faida kwenye biashara au uwekezaji wao.

    Inakadiriwa kuwa mwaka huu China itachukua nafasi ya Marekani kuwa soko kubwa zaidi la matumizi kote duniani, hali inayomaanisha kuwa China itakuwa soko linalogombewa kwa nguvu zote na makampuni ya kimataifa, yakiwemo yale ya Marekani.

    Serikali ya Marekani imeanzisha vita ya kibiashara dhidi ya China kwa kisingizo cha kulinda maslahi yake, lakini je hatua hizo za upande mmoja zitayanufaisha kivipi makampuni ya Marekani yaliyopata faidi kubwa kutokana na biashara zao nchini China?

    Ni maoni ya pamoja kwenye jumuiya ya kimataifa kwamba, vita ya kibiashara huleta hasara, na wala sio manufaa, kwa pande zote mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako